Story by Our Correspondents –
Baadhi ya Mawakili katika ukanda wa Pwani wamesisitiza haja ya kufanyiwa kwa marekebisho ya sheria za umiliki wa ardhi nchini.
Wakiongozwa na Wakili George Kithi, mawakili hao wamesema mfumo unaotumika kwa sasa wa umiliki wa ardhi unazidi kuwakandamiza wakaazi wa Pwani.
Akizungumza katika eneo la Shariani kaunti Kilifi, Wakili Kithi amesema kufanyiwa kwa marekebisho kwa sheria hizo kutasitisha mizozo ya ardhi pamoja na kulikabili swala la uskwota kanda ya Pwani.
Hata hivyo amewarai wakaazi wa eneo la Shariani na kaunti nzima ya Kilifi kuunga mkono azma yake ya kuwania kiti cha useneta kaunti ya Kilifi akisema mabadiliko mengi ya uongozi huchangiwa na viongozi waadilifu.