Picha kwa hisani –
Baada ya mwanamuziki wa Bongo Flava, Rich Mavoko, kukaa kimya wa muda mrefu hatimaye, amejitokeza mtandaoni akiwa na habari njema kwa mashabiki wake kuhusiana na muziki wake.
Mavoko amejitokeza mtandaoni baada ya ukimya usiopungua miezi 7, ambapo mara ya mwisho kupost kupitia akaunti yake ya mtandao wa Instagram, ilikuwa ni tarehe 1 mwezi January, mwaka huu. Hii ni baada ya tetesi kuenea katika mitandao ya kijamii kwamba ameshindwa na kuacha muziki baada ya kutoka katika recording label ya WCB na kuona kwamba kazi zake hzifanyi vyema kama hapo awali.
Kupitia ukurasa huo, Mavoko ametangaza ujio wake mpya unaombata na wimbo wake mpya ‘Minitape’ atakaouachia tarehe 7, mwezi huu. Mavoko aliwashukuru mashabiki wake wanaomjali na ambao walimtafuta kipindi hiki alipokuwa kimya wakimrai atoe kazi zingine mpya. Pia aliwashukuru kwa uvumilivu.
Hata hivyo, msanii huyo aliwahakikishia mashabiki wake kuwa anapenda muziki na hayuko tayari kutoka kwa sanaa hiyo.