Visa vya Wazee kuuawa katika Kaunti ya Kilifi vimeonekana kurudi upya na mara hii vimeripotiwa kufanyika mchana.
Kulingana na Mshirikishi wa shirika la HAKI YETU Julius Wanyama mauaji hayo sasa yamezua hofu miongoni mwa wazee wakongwe ambao ndiyo walengwa wakuu
Mshirikishi Wanyama ametaja kuwa licha ya maafisa wa usalama kupambana na wahalifu wanaotekeleza visa hivyo bado vimeonekana kuongezeka .
Shirika hilo sasa limeiomba serikali kupitia mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya ummaa nchini Noordin Hajj pamoja na mkuu wa kitengo cha upelelezi nchini George Kinoti kusaidia katika kusuluhisha mauaji hayo .