Picha Kwa Hisani –
Waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiangi,inspekta jenerali Hilary Mutyambai na mkurugenzi wa idara ya DCI George Kinoti wamefika mbele ya kamati ya bunge la seneti kuhusu usalama kuhojiwa kuhusiana na kutiwa nguvuni kwa maseneta watatu siku ya juma tatu juma hili.
Hata hivyo waandishi wa habari wamezuiliwa kufatilia kikao hicho baada ya mwenyekiti wa kamati hio seneta Yusuf Hajji kuwataka wanahabari kuondoka katika eneo hilo kwa misingi kwamba hawakupewa mualiko.
Watatu hao wanahojiwa ili kueleza chanzo cha kutiwa nguvuni kwa maseneta watatu akiwemo wa Kakamega Cleophas Malala,Christopher Langat wa Bomet na Steve Lelegwe wa Samburu.
Itakumbukwa kwamba Matiang’i na Mutyambai walikosa kufika mbele ya kamati hio siku ya jumatatu juma hili kama walivyoagizwa na maseneta.