Picha kwa hisani –
Waziri wa usalama wa ndani dkt Fred Matiang’i amewaagiza maafisa wa usalama walioko likizo msimu huu wa sherehe za mwisho wa mwaka kurejea kazini.
Akitoa tangazo hilo hapo jana baada ya kuzuru makao makuu ya maafisa wa kitengo cha RDU huko Embakasi,Matiangi amesema hatua hio inalenga kuhakikisha taifa lina usalama wa kutosha msimu huu wa sherehe.
Kwenye hotuba yake Matiangi vile vile amesema maafisa wa polisi wanaopiga doria msimu huu wa krismasi na mwaka mpya hawatowakabili wahalifu pekee,bali hata raia watakaovunja sheria za kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.
Matiangi ameapa kuzuru maeneo mbali mbali ya taifa msimu huu wa sherehe za mwisho wa mwaka ili kukagua hali ya usalama katika maeneo hayo,akiwasihi wakenya kuhakikisha wanazingatia sheria za nchi ili wasijipate pabaya.