Story by Bakari Ali
Waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang’i ameitaka taasisi ya uhasibu nchini ICPAK kushirikiana na idara mbalimbali za serikali kufanikisha vita dhidi ya ufisadi nchini.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa wakati wa kongamano la 39 la taasisi hiyo, Matiang’i amesema ni lazima taasisi ya ICPAK ishirikiane na idara husika za serikali kukabiliana na ufisadi ambao umeathiri uchumi wa taifa.
Dkt Matiangi amesema wahasibu wana mchango mkubwa katika kuimarisha uchumi wa taifa, akisema huu ni wakati mwafaka wa wao kushirikiana na idara za serikali katika mipangilio yote ya ugavi na utumizi wa fedha za umma.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa taasisi hiyo ya ICPAK mhasibu George Mokuwa amesama taasisi hiyo itashirikiana vilivyo na serikali ili kuimarisha uchumi wa taifa hususan baada ya janga la virusi vya Covid 19 kuathiri sekta mbali mbali za kiuchumi nchini.