Story by Our Correspondents –
Waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang’i amewaonya wanasiasa dhidi ya kuendeleza siasa za chuki na uchochezi nchini, akisema kiongozi atakayepatikana akiwachochea wananchi atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Waziri Matiang’i amewataka viongozi wa kisiasa kukoma kuendeleza siasa za chuki, akisema hatua hiyo huenda ikachangia migawanyiko ya kisiasa na kikabila miongoni wa jamii.
Akizungumza katika kaunti ya Nyamira, Waziri Matiang’i amesisitiza kuwepo kwa amani nchini huku akiwahakikishia wananchi kwamba serikali imeweka mikakati mwafaka ya kuhakikisha wakenya wanaishi bila ya hofu yoyote.
Wakati uo huo amewataka vijana kukoma kutumiwa vibaya na baadhi ya watu wenye malengo potovu kwa taifa hili, akisema vijana ndio nguvu kazi ya taifa.