Story by Our Correspondents –
Waziri wa usalama wa ndani nchini Dkt Fred Matiang’i amewakosoa baadhi ya viongozi wa kisiasa nchini dhidi ya tabia ya kuingilia utendakazi wa maafisa wakuu serikalini.
Akizungumza katika mkutano wa kiusalama katika kaunti ya Nyamira, Matiang’i amesema ni jambo la kushangaza kuona baadhi ya wanasiasa wakiwakosoa na kuwashambulia kwa maneno maafisa wa serikali.
Matiang’i amesema ni jukumu la viongozi hao kuheshimu utendakazi wa maafisa wa serikali wanaowajibika kuhakikisha taifa hili linapiga hatua kimaendeleo huku akishikilia kwamba kila wanasiasa anafaa kukambana na hali yake.
Wakati uo huo ameahidi kwamba serikali kupitia Wizara ya usalama wa ndani itahakikisha usalama unaimarishwa zaidi kabla ya uchaguzi na hata baada ya uchaguzi.