Story by Our Correspondents –
Waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang’i ametangaza ramsi kuwa tarehe 11 mwezi Oktoba itakuwa sikukuu ya kitaifa ya kuadhimisha siku Utamaduni.
Waziri Matiang’i amesema tangazo hilo limechapishwa rasmi katika gazeti la serikali ambapo sikukuu hiyo itakuwa ikiadhimishwa kila tarehe 10 mwezi Oktoba kila mwaka lakini mwaka huu itasheherekewa tarehe 11 mwezi Oktoba kutokana na kwamba tarehe 10 itakuwa siku ya Jumapili.
Matiang’i ametangaza rasmi tangazo hilo kwa kuzingatia sehemu ya pili na ile ya nne ya katiba ya nchi kuhusu sikukuu za kitaifa na sikukuu hiyo itaandaliwa kwa mara ya kwanza kote nchini.
Wakati uo huo amedokeza kuwa wakenya watatumia sikukuu hiyo katika kuadhimisha tamaduni zao na kuchangia umoja, uwiano wa kitaifa na kuimarisha uchumi wa nchi.