Story by Our Correspondents –
Waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang’i ametangaza rasmi kwamba siku ya Jumatatu ya tarehe 13 mwezi huu itakuwa siku ya kitaifa ya mapumziko kwani sherehe za Jumhuri za mwaka kuu zitaadhimisha siku ya Jumapili ya tarehe 12.
Katika tangazo hilo lililochapishwa rasmi katika gazeti la serikali Waziri Mataing’i amesema kulingana na sehemu ya pili na nne ya sheria za sherehe za kitaifa sawa na kifungu cha 110, siku ya Jumatatu itakuwa siku ya mapumziko.
Matiangi ameweka wazi kwa sherehe hizo zitaandaliwa katika bustani ya Uhuru jijini Nairobi na zitaongozwa na Rais Uhuru Kenyatta huku wakenya watakaojitokeza kuhudhuria sherehe hizo wakihimizwa kuzingatia kanuni za Covid-19.
Wakati uo huo amewahimiza wakenya kusheherekea sherehe za Jamhuri kwa kutambua umoja, mshikamano wa taifa na kujenga uchumi wa nchi kwani taifa litakuwa linaadhimisha miaka 58 ya uhuru.