Story by Our Correspondents-
Waziri wa usalama ndani Dkt Fred Matiang’i amesema Serikali inafuatilia kwa kina mashirika yasiokuwa ya kiserikali ambayo hayajasajiliwa ili kuhakikisha yanasajiliwa na kuzuia kutumika kwa shughuli za ugaidi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti kuhusu sekta ya mashirika yasiokuwa ya serikali jijini Nairobi, Waziri Matiang’i ameiagiza bodi inayosimamia mashirika hayo kuchukua jukumu la kuyasajili mashirika ambayo hajasajiliwa katika kipindi cha miezi mitatu.
Waziri huyo wa usalama hata hivyo ameyataka mashirika hayo kujitenga na wanasiasa wasio na malengo bora kwa wananchi, akisema hatua hiyo itazuia kushuhudia kwa siasa za vurugu.
Wakati uo huo ameahidi kwamba serikali itakahakikisha inatekeleza wajibu wake wa kuwalinda wananchi ili kuhakikisha taifa hili linashuhudia amani.