Msanii wa Bango kutoka Presto Sounds, Matano Jnr amefunguka na kutueleza kuwa amepata baraka tele msimu huu.
Akizungumza na Dominick Mwambui kwenye kipindi cha Misakato Ya Bango, Matano amesema kuwa yeye na mpenzi wake wantarajia watoto mapacha.
“Ni hali ambayo sikuitarajia kusema ukweli lakini nilijawa na furaha isiyokuwa na kifani nilipobaini kuwa mke wangu alikuwa ni mja mzito wa mapacha, “amesema Matano.
Baada ya furaha hiyo ameamua kumtunuka mke wake kibao ambacho atakiwachilia rasmi hivi karibuni.
“Ili kumuonyesha mapenzi zaidi mke wangu nimemwandikia wimbo ambao nitauwachilia hivi karibuni kwa jina Kadede,” ameongezea Matano.