
Mkurugenzi wa idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini Bi Stela Aura.
Serikali za mataifa ya IGAD zimehimizwa kuzingatia utabiri wa hali ya hewa katika mpangilio wake ili kuepukana na maafa na hasara inayopatikana kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Akizungumza katika Makala ya 54 ya kongamano la kuthathmini mwelekeo msimu wa Machi, Aprili,Mei (MAM) utakavyokuwa, katibu katika wizara ya mazingira na misitu, Mohammed Elmi, amesema kuwa mabadiliko ya tabia nchi yameathiri pakubwa usalama wa chakula.
Kulingana na Elmi watu milioni 25 katika mataifa ya IGAD wanakumbwa na ukosefu mkubwa wa chakula hali aliyoitaja kuwa inaweza kutatuliwa iwapo utabiri wa hali ya hewa utatiliwa manani katika mipangilio ya kilimo.
Naye mkurugenzi wa idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini Bi Stela Aura amesema kuwa watu takriban 236 walifariki mwaka jana kutokana na kupuuzwa kwa utabiri wa hali ya hewa. Jambo analosema linaweza kuepukwa iwapo utabiri wa hali ya hewa utachukuliwa kwa umuhimu mkubwa.