Picha kwa hisani –
Kenya imejiunga na mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha siku ya ugonjwa wa saratani hii leo.
Kwenye ripoti ya mwaka 2020 iliyotolewa na shirika la afya duniani WHO,shirika hilo limetoa wito wa asilimia 70 ya wanawake kupimwa saratani ya kizazi wanapofikisha umri wa miaka 35.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus aidha ameseme wanawake pia wanapaswa kupimwa tena saratani ya kizazi wanapofikisha umri wa miaka 40.
Itakumbukwa kwamba mwaka uliopita WHO ilizindua mkakati mpya wa kupambana na kuiangamiza Saratani ya kizazi, kwa matumizi ya chanjo, vipimo vipya na matibabu ili kuokoa maisha ya watu kufikia mwaka 2050.