Mastar Kimbo sio mgeni kwa wengi, ni msanii anayejulikana kwa mziki aina ya Rap.
Miongoni mwa kazi alizofanya ni kibao English Gold kilichompatia umaarufu mkubwa kufikia sasa.
Kando ya kuwa na mawimbi makubwa kwenye mziki, Mastar Kimbo sasa anavurumisha wimbi lingine. Wimbi la kuihamasisha jamii dhidi ya virusi vya HIV.
Kwa sasa yupo chini ya Shirika la Connect to Retain mjini Kilifi linalojihusisha na kuwasaidia vijana walioathirika na virusi vya HIV vinavyosababisha UKIMWI.
“Kipenzi chetu, mwenye kupewa milki ya kipawa chakuimba alikua mzimamzima akituburudisha ndani ya YEAH event. Master kimbo will always be part of us and we are walking with him sako kwa bako,” umesema ujumbe kwenye ukurasa wa Connect To Retain.