Katibu mkuu msimamizi katika wizara ya ardhi, Gideon Mung’aro. Picha/kwa hisani
Wizara ya ardhi nchini inalenga kuwajumuisha masorovea wa kibinafsi katika wizara hio kwa lengo la kuboresha utendakazi wa wizara hiyo.
Katibu mkuu msimamizi katika wizara ya ardhi Gideon Mung’aro amesema wizara ya ardhi nchini inakumbwa na uhaba wa masorovea hali inayolemaza utekelezwaji wa miradi ya kimaendeleo nchini.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la 50 la shirika la masoroveya nchini huko diani kaunti ya Kwale Mung’aro amedokeza kwamba wizara hio pia inalenga kutoa huduma kwa wananchi kupitia mfumo wa kidigitali.
Kwa upande wake mwenyekiti wa masorovea nchini Abraham Samoei amesema wataikagua upya sheria ya ardhi ili kuona kwamba inamfaidi mwananchi.
Taarifa na Salim Mwakazi.