Zaidi ya maskwota elfu 3 katika ardhi ya Nguu tatu kule Kisauni kaunti ya Mombasa wameshikilia msimamo wao kuwa hawataruhurusu Shirika la Bandari Sacco linalodai kumiliki kipande hicho cha ardhi kujenga ukuta kwenye ardhi hiyo.
Wakiongozwa na Mwenyekiti wao Martin Chiponda, maskwota hao wameeleza kughadhabishwa na hatua ya idara ya usalama eneo hilo, kutaka kujengwa ukuta huo licha ya serikali ya kaunti ya Mombasa kuweka wazi kuwa ni kinyume cha sheria.
Akizungumza kwenye mkao uliowaleta pamoja maskwota hao na idara ya usalama eneo hilo, Chiponda amesema tayari wamewasilisha kesi kwenye Makahakama ya upeo nchini kupinga ujenzi wa ukuta huo huku akimtaka Naibu Kamishina wa Kisauni Kipchumba Ruto kutatua swala hilo.
Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Kisauni Kipchumba Ruto amezitaka pande zote mbili kutumia sheria katika kusulughisha mzozo wa ardhi hiyo.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.