Taarifa na Sammy Kamande.
Kiongozi wa walio wachache bungeni John Mbadi ameyataka mashirika ya ukaguzi wa ndani kusaidia serikali katika kupambana na ufisadi humu nchini.
Akizungumza mjini Mombasa, Mbadi amesema mashirika hayo ya ukaguzi yamekuwa wakiwatoa watu wafisadi kutoka kwa mashirika mbalimbali ambayo bilioni zao ziliporwa.
Mbadi amesema ipo haja ya jamii kufundishwa umuhimu wa ukaguzi huo ili kuhakikisha hakuna ubadhirifu wowote wa fedha na mali ya umma.
Wakati uo huo amedai kuwa kuporwa kwa fedha za umma katika serikali kuu na zile za kaunti ni kutokana na tamaa za baadhi ya viongozi nchini.