Story by Ali Chete-
Mkurugenzi wa bodi ya mashirika yasiokuwa ya kiserikali David Ole Sankoki ameyataka mashirika hayo kutumia vyema fedha wanazopata kutoka kwa wafadhili.
Akizungumza na Wanahabari katika kaunti ya Mombasa wakati wa kuadhimisha wiki ya mashirika yasiokuwa ya kiserikali, Sankoki amesema baadhi ya mashirika hayo hutumia fedha hizo kwa manufaa ya watu wachache.
Sankoki ameyaonya mashirika hayo dhidi ya kutumika katika uhalifu na mataifa ya kigeni, akisema shirika litakalo patikana na kashfa hizo litapokonywa vyeti vyake na kuchukuliwa hatua.
Kwa upande Habib Hakim kutoka shirika la Helping Hands Pwani amesema kuna baadhi ya mashirika yanayotumia majina ya mashirika mengine kupata fedha na kuitaka bodi hiyo kuingilia kati swala hilo.