Story by Ali Chete-
Mashirika ya kijmii katika ukanda wa Pwani wameitaka Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC na idara ya upelelezi wa jinai nchini DCI pamoja na maafisa wa usalama kushirikiana na kuhakikisha uchaguzi mkuu wa Agosti 9 unafanyika kwa amani.
Mashirika hayo yakiongozwa na mkurugenzi mkuu wa Shirika la Sisters For Justice Naila Abdallah, wamesisitiza haja ya idara hizo pamoja na Tume ya kitaifa ya uwiano na utangamano NCIC kuchunguza semi za uchochezi zinazoendelezwa na wanasiasa na kuwachukulia hatua.
NAILA – IDARA 08 04 22
Wakizungumza na Wanahabari katika kaunti ya Mombasa, Naila amewataka wanasiasa wanaowania nyadhfa mbalimbali za kisiasa nchini kukoma kuwachochea wananchi na kuwagawanya kwa mirengo ya kisiasa.
NAILA – WANASIASA 08 04 22
Ni kauli zilizoungwa mkono na Afisa wa maswala ya dharura katika Shirika la MUHURI Francis Auma aliyesema kuna baadhi ya maafisa wanaochunguza visa vya uchochezi kwa wanasiasa na lazima washusika watachukuliwa hatua.