Mashirika ya kijamii katika kaunti ya Mombasa yamewalaumu wanawake kwa kuchangia ghasia wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu nchini.
Mashirika hayo yakiongozwa na lile la KECOSCE chini ya afisa wa nyanjani Mwalimu Rama, wamesema wanawake wamejiweka katika mirengo mbalimbali ya kisaisa na kuchangia pakubwa vijana kuzua ghasia wakati za kampeni za uchaguzi.
Mwalimu amesema shirika hilo linashirikiana na idara ya usalama kuhakikisha mikakati mwafaka ya kuhamasisha vijana kujitenga na vurugu inafaulu.
Kwa upande wake Naibu Kamishna wa gatuzi dogo la Kisauni Jamleck Mbuba amesema ushirikiano mwema kati ya jamii, mashirika ya kijamii na idara ya usalama umepiga hatua katika kuyadhibiti magenge ya kihalifu.