Taarifa na Alphalet Mwadime.
Watetezi wa haki za kibinadamu Ukanda wa Pwani wataungana na wenzao kutoka sehemu nyingine za nchi kuandama ili kuwashinikiza Wabunge kuwachana na azma yao ya kupigania nyongeza ya mishahara.
Afisa wa maswala ya dharura katika Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu nchini la Haki Afrika Mathias Shipetta amesema kwamba bila ya watetezi hao kushirikiana na wananchi na kufanya harakati hizo iwapo mwananchi mashinani atazidi kukandamizwa na wabunge hao walafi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Hussein Khalid amekariri kwamba tayari Shirika hilo linashirikiana na watetezi wengine wa haki za kibindamu ili kulijadili swala hilo na Wabunge wa eneo la Pwani ili kuwashinikiza kulitupilia swala hilo.