Mashirika sita ya utetezi wa haki za kibinadamu pwani yanapanga kukutana na rais Uhuru Kenyatta ili kumkabidhi mapendekezo yao kuhusiana na swala la mauaji ya kiholela na kutoweka kwa raia pwani.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la utetezi wa haki za kibinadamu nchini la Haki Afrika Hussein Khalid amesema mashirika husika yatafanya matembezi kutoka Mombasa hadi ikulu ya rais ya jijini Nairobi ili kumkabidhi rais Uhuru Kenyatta matakwa yao.
Mashirika hayo ni Human Development Agenda, Shirika la Wanawake wa Kiislamu KEMWA, Sauti ya Wanawake, Kituo cha Sheria na Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu la Kwale Human Rights Network
Msafara huyo unatarajiwa kung’oa nanga mwezi ujao wa Novemba.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.