Picha kwa Hisani –
Baadhi ya maseneta nchini wamepuuzilia mbali madai yanayoenezwa kuwa mvutano wa mfumo mpya wa ugavi wa raslimali kwa serikali za kaunti unaoshudiwa kwa sasa umeingizwa siasa.
Wakiongozwa na Seneta wa kaunti ya Kwale Isaa Juma Boi, viongozi hao wamesema taifa hili ni lazima lisimame pamoja katika ugavi sawa wa raslimali kwani wananchi wanahitaji maendeleo mashinani.
Kwa upande wake Seneta wa Mombasa Mohammed Faki amesema tatizo la kucheleweshwa kwa fedha za kaunti halijachangiwa na maseneti bali limekupo kwa muda.
Naye Seneta Maalum Abshiro Halake amewataka magavana kusimama na bunge la Seneti wakati huu ambao wanapigania mgao zaidi wa fedha.