Story by Hussein Mdune –
Viongozi mbalimbali humu nchini wamejitokeza na kukashfu vikali utendakazi idara ya usalama kwa kile wanachokitaja kama imekosa kuwajibikia majukumu yake ipasavyo.
Akizungumza katika kikao cha bunge la Seneti wakati wa hoja ya swala la usalama wa nchi, Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen amesema licha ya maafisa wa polisi kushutumiwa kwa visa mbalimbali vya uhalifu hakuna hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa.
Naye Seneta wa Mombasa Mohammed Faki amesema swala la ukosefu wa usalama katika kaunti ya Mombasa na Pwani kwa jumla limekuwa kero huku akitaka swala hilo kujadiliwa na kamati ya haki na sheria nchini.
Kauli yake imeungwa mkono na Seneta wa Kakamega Cleopas Malala aliyesema kuna haja ya kuangalia upya kwa mfumo wa masomo wa maafisa wa usalama hususan katika chuo cha mafunzo ya polisi cha kiganjo.