Picha kwa hisani
Mvutano unaendelea kushuhudiwa katika bunge la Seneti kuhusiana na hoja ya kujadili mfumo mpya wa ugavi wa fedha zinazotengewa serikali za kaunti baada ya Seneti wa Siaya James Orengo kupendekeza kuhairishwa kwa kikao hicho.
Hatua ya Seneta Orengo imetokana na kushuhudiwa kutoafikiana kwa maseneta kuhusu mfumo huo umpya wa ugavi wa mapema, wengine wakiunga mkono huku wengine wakiupinga kwa misingi kwamba utahujumu maendeleo ya kaunti.
Hata hivyo ilimlazima spika wa bunge hili Ken Lusaka kutumia kipengele cha 105 cha vikao vya bunge na maseneta kupiga kura kuendelea kujadiliwa kwa hoja hiyo hadi mwafaka upatikane.
Kwa sasa kikao hicho cha kujadili hoja ya mfumo mpya wa ugavi wa mapato nchini kinaendelea huku maseneta wakitofautiana kuhusiana na mapendekezo ya Tume ya ugavi wa mapato nchini CRA.