Picha kwa hisani –
Maseneta wameshikilia msimamo wa kutumia mfumo wa zamani wa ugavi wa mapato nchini huku wakiahidi kupitisha mswada wa awali wa ugavi wa mapato bungeni siku ya Jumanne wiki ijayo katika kikao cha nane za kujadili mswada huo.
Wakiongozwa na Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen, maseneta hao wameafikia kuunga mkono hoja ya Seneta wa Meru Mithika Lunturi pamoja na kuafikia kutengwa kwa shilingi bilioni 250 hadi bilioni 270.
Katika kikao na Wanahabari, Murkomen amesema masenata wanaendelea na majadiliano kuhusu mfumo wa ugavi wa mapato nchini na kikao cha wiki ijayo itaibuka na mwafaka wa mzozo huo.
Wakati uo huo amedai kama maseneta watafanya kila juhudi kuhakikisha wanatetea haki za wananchi mashinani huku akiwataka maseneta kuonesha uongozi bora.