Picha kwa Hisani –
Bunge la Seneti limepiga kura kuendelea kujadiliwa kwa mswada wa mfumo mpya wa ugavi wa mapato hadi mwafaka upatikane kwa kura 31 dhidi ya 28 baada ya hoja ya kuairishwa kwa kikao hicho kutokana na kuzuiliwa kwa maseneta watatu kukosa kuafikiwa alasiri ya leo.
Spika wa bunge hilo Ken Lusaka ameamuru mswada huo kuendelea kujadiliwa bungeni hadi mwafaka upatikane kwa kuzingia Katiba ya nchini vipengele ya bunge ikiwemo kipengele cha 123 kinachompa nguvuni ya kufanya uamuzi.
Akichangia katika hoja hiyo ya kabla ya maseneta kupiga kura, Seneta wa Kwale Issah Boi amesema ni makosa makubwa kwa maseneta wanaofaa kuhudhuria vikao vya bunge na kujadili mswada muhimu wakionekana kuwatia nguvuni na polisi.
Naye Seneta wa kaunti ya Tana river Wario Ali amesema japo kaunti zaidi ya 29 zitateseka iwapo mswada huo umepitishwa, akihoji kuwa ni makossa bunge kuendelea na mswada huo umuhimu ilhali wengine wanazuiliwa na polisi.
Kwa upande wake Seneta wa Mombasa Mohamed Fakii ametetea kuachiliwa kwa maseneta watatu waliotiwa nguvuni na polisi, akisema hatua iliochukuliwa na maafisa hao ni kinyume cha sheria.
Hata hivyo Seneta wa Isiolo Fatuma Dullo, amesema japo anaunga mkono serikali katika kufanikisha maswala mbalimbali nchini, iwapo mswada huo utapitshwa basi kaunti nyingi ikiwemo ya Isiolo itapoteza pesa nyingi.
Maseneta hao waliotiwa nguvuni na polisi na kutarajiwa kufikishwa Mahakama hapo kesho ni pamoja na Seneta wa Kakamega Cleophas Malala, Seneta wa Bomet Christopher Lang’at na Seneta wa Samburu Steve Lelegwe