Picha kwa hisani –
Bunge la Seneti limepiga kura kwa kauli moja na kuusuluhisha mvutano wa ugavi wa raslimali kwa serikali za kaunti nchini uliozua mdahalo kwa vikao 10 katika bunge hilo.
Wabunge hao wamepiga kura kwa kauli moja baada ya Kamati maalum ya maseneta 12 waliotikwa jukumu la kuibuka na mwafaka wa mfumo wa ugavi wa raslimali kwa kaunti inayoongozwa na Seneta wa Nairobi Johnson Sakaja na mwenzake wa Bungoma Moses Wetangula kuwasilisha ripoti yao bungeni.
Awali akiwasilisha ripoti ya mwafaka huo mbele ya bunge la Seneti alasiri ya leo, Mwenyekiti wa kamati hiyo Johnson Sakaja, amesema wameafikia maswala manane muhimu yatakayosaidia serikali za kaunti kuendeleza shuhuli zao.
Hata hivyo katika mwafaka huo, kaunti ya Nairobi imenufaika zaidi kwa kutengewa kiwango cha juu cha shilingi bilioni 3.3 na kupelekea mgao wa kaunti hiyo kuwa shilingi bilioni 19.
Kaunti ya Lamu sasa itafikia shilingi bilioni 3.1, kaunti ya Tharaka Nithi ikipokea nyongeza ya chini ya shilingi milioni 286 huku kamati hiyo ikiafikiana kuwa hakuna kaunti itakayopunguziwa katika mfumo huo mpya