Kwenye Picha – Bi Khamisa Maalim Zajjah
Licha ya Serikali ya kitaifa na zile za kaunti kushinikizwa kuyaangazia masaibu yanayowakumba walemavu humu nchini, kilio hicho kimeonekana kupuuzwa.
Mwenyekiti wa makundi mbalimbali ya walemavu katika Ukanda wa Pwani Bi Khamisa Maalim Zajjah amesema walemavu wanataabika hasa baada ya taifa hili kukumbwa na virusi vya Corona.
Zajjah ameyasema hayo alipozikimu zaidi ya familia 100 za watu walio na ulemavu kwa chakula na vifaa vya kujikinga na Virusi vya Corona katika mtaa wa vitongoji duni wa Hodihodi eneo la Shanzu kaunti ya Mombasa ambapo amesema jamii hiyo inahitaji msaada.
Kwa upande wake Emilly Likhodito waliofaidika na msaada huo, ameitaka Serikali kuwatambua katika misaada mbalimbali ya kibinadamu wakati huu wa janga la Corona.