Hakuna mtoto yeyote atakayeruhusiwa kusalia katika fuo za bahari hindi baada ya saa kumi na mbili jioni msimu huu wa likizo ya mwisho wa mwaka.
Akitoa amri hiyo mjini Mombasa, Kamishna wa kaunti ya Mombasa Evans Achoki amesema hali hiyo imewaweka watoto wengi katika hatari ya kupotoka kimaadili na kushiriki ngono za kiholela katika fuo za bahari hindi.
Achoki amesema maafisa wa usalama watakuwa kwenye minara maalum itakayojengwa katika ufuo wa Shelly eneo la Likoni na ufuo wa bahari ya ‘Pirates’ kule Bamburi ili kuchunguza wanaoshiriki visa vya utovu wa maadili.
Wakati uo huo amewataka wale wote watakaohangaishwa na wahudumu katika maeneo ya bahari hindi kuripoti mara moja ili wahalifu hao wakabiliwe.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.