Kamishna wa kaunti ya Kwale Karuku Ngumo ameonya kuwa mtoto yoyote atakayepatika katika maeneo ya fuo baada ya saa kumi na mbili jioni msimu huu wa likizo na siku kuu ataadhibiwa vikali.
Ngumo amewahimiza wazazi kuwajibika kwa kuwalinda wana wao ili kuwaepusha na maovu mbali mbali akisema wazazi ambao watoto wao watapatikana wakirandaranda katika sehemu za fuo watafunguliwa mashtaka kwa kutowajibikia majukumu yao ya ulezi.
Afisa huyo tawala ametoa onyo hilo wakati huu ambapo msimu wa siku kuu ya krismasi unawadia na wasanii wengi kutoka Afrika mashariki wanazuru humu nchini kutumbuiza mashabiki wao mbali mbali.
Aidha amewaonya maafisa wa usalama waliotwikwa jukumu la kushirika doria sehemu za fuo, kutekeleza majukumu yao vyema akionya kwamba afisa ambaye ataruhusu watoto kurandaranda ovyo katika sehemu za fuo bada ya saa zilizoruhusiwa ataadhibiwa pia.
Taarifa na Salim Mwakazi.