Story by: Mwahoka Mtsumi
Serikali imeweka wazi kwamba Wizara mbalimbali nchini, idara za kiserikali na taasisi nyingenezo zinadaiwa zaidi ya shilingi bilioni 80 kufikia Disemba 31 mwaka wa 2022.
Mdhibiti wa bajeti nchini Margaret Nyakang’o amefichua kwamba kufikia Juni 30 mwaka wa 2022 taasisi hizo zilikuwa zinadaiwa shilingi bilioni 83.98 kati ya shilingi bilioni 62.8 zilizokuwa za matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 21.2 za matumizi ya maendeleo.
Margaret amesema kulingana na ripoti iliyotolewa taasisi hizo zimelipa deni la shilingi bilioni 3.6 ambayo ni asilimia 4.4 pekee ya deni hilo na kubakisha shilingi bilioni 80.3.
Katika ripoti hiyo, Margaret amesema juhudi zinazoendelezwa na Rais William Ruto za kuinua uchumi wa nchi, huenda deni hilo litakamilishwa kulipwa na kumuwezesha mkenya mlipa ushuru kumudu gharama ya maisha.