Story by Our Correspondents-
Viongozi wa mataifa 7 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatarajiwa kukutana jijini Nairobi kujadili hali ya usalama katika maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mkutano huo ambao unatarajiwa kuongozwa na Rais Uhuru Kenyatta ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo katika Ikulu ya Nairobi umejiri wakati ambapo mapigano makali yanaendelea kushuhudiwa kati ya Kinshasa na Kigali.
DRC imekuwa kiilaumu serikali ya Rwanda inayoongozwa na Rais Paul Kagame ikidai kwamba imekuwa ikifadhili kundi la waasi la M23 ili kutatiza usalama wa taifa la Congo hali ambayo imechangia kushuhudiwa kwa uhasama wa kidiplomasia kati ya Kinshana na Kigali.
Hata hivyo Rwanda imekanusha madai ya kuwaunga mkono waasi hao huku nchi zote mbili zikilaumiana kwa kufanya mashambulizi ya kuvuka mpaka hali ambayo imechangia viongozi hao kuitisha mkutano huo ili kuibuka na suluhu la amani.