Waziri wa Utalii nchini Najib Balala amesema mapato ya sekta ya Utalii yaliongezeka kwa asilimia 22 katika mwaka uliopita wa 2018.
Akiongea mjini Mombasa, Waziri Balala ameeleza kuwa katika mwaka wa 2018, Kenya iliweza kukusanya takriban shilingi bilioni 157, akisema kuwa kiwango hicho ni ishara ya kuboreshwa kwa sekta ya utalii nchini.
Waziri Balala amesema serikali itaendelea kuwekeza zaidi katika sekta hiyo, kwa kuvumbua na kuvifanyia ukarabati vivutio vya watalii nchini.
Ametoa mfano wa eneo la Mamangina Drive jijini Mombasa ambalo linafanyiwa ukarabati na serikali kupitia wizara ya utalii.
Taarifa na Michael Otieno.