Maofisaa wa polisi wafisadi wanaofanya kazi katika eneo la Magarini kaunti ya Kilifi huenda wakapoteza kazi zao baada ya Naibu Rais William Ruto kuitisha majina yao.
Akizungumza huko Magarini wakati wa kupeana kwa hati miliki za ardhi, Ruto amesema kuwa amepokea malalamishi kutoka kwa Mbunge wa eneo hilo Michael Kingi.
Ruto amekiri kuwa atashughulikia swala hilo kwa haraka ili kuhakikisha kuwa maofisaa wafisadi wanaondolewa katika eneo hilo.
Taarifa na Radio Kaya.