Mwakilishi wa wadi ya Mwereni katika kaunti Kwale Manza Beja amekosoa pendekezo la serikali ya kaunti ya Kwale la kutaka kuteleleza ugavi wa ardhi ya jamii katika wadi hiyo ya Mwereni Ranchi.
Manza amesema makubaliano ya hapo awali ilikuwa kwanza kuwepo na mazungumzo kati ya viongozi wa kaunti ya Kwale na wakaazi wa eneo hilo kabla ya mpango wa ugavi wa ardhi hiyo kuanza.
Kiongozi huyo amesema ardhi hiyo ina raslimali nyingi za jamii na ni lazima kuwepo na mazungumzo kabla ya serikali ya kaunti hiyo kuanza zoezi la ugavi wa ardhi hiyo, akihoji kuwa kwanza swala la mipaka linafaa kuangaziwa na mpango wa ugavi wa ardhi kuwekwa kando.