Timu ya Manuari FC imeibuka na ubingwa wa ligi ya mheshimiwa Mwerupheh Ndoro baada ya kuichapa Welerys FC kutoka Kilindini mabao 3-1 mechi iliyochezwa katika uga wa shule ya msingi ya Mtsamvyani, wadi ya Mkongani.
Mabingwa hao walitia kibindo kitita cha Ksh 30,000 , kikombe na jezi,huku mshindi wa pili akipata ksh 15,000 pamoja na jezi nao Eleven stars wakapata jezi na Ksh 7,500 kama mshindi wa tatu.
Mhandisi Lung’nzi Chai ni miongoni mwa wageni waliohudhuria mchuano huo uliyowavutia wenyeji wa sehemu hiyo.
Taarif na Radio Kaya.