Obado alazwa hospitalini
Gavana Okoth Obado amelazwa katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta hapa Nairobi.Ni baada ya kuugua akiwa gerezani Industrial Area.Obado ambaye yadaiwa anaugua malaria, alipelekwa hospitalini humo kwa gari la kibifnasi.Obado yuko rumande akisubiri hatma yake iwapo ataachilwia kwa dhamana au la, na jaji Jessi Lessit tarehe nane mwezi huu.Anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kinyama ya Sharon Otieno.
Malumbano yanukia kati ya wizara ya kilimo na fedha
Malumbano yananukia kati ya wizara ya fedha na ile ya kilimo, baada ya waziri wa fedha Henry Rotich kujitenga na hali kwamba wakulima wa mahindi bado hawajapokea fedha zao.Rotich anasema shilingi hizo bilioni 1.4 zilikabidhiwa wizara ya kilimo.Wakulima walitazamiwa kupokea malipo kuanzia jumatatu kwa mahindi waliyouzia serikali mwaka jana na sasa wanakadiria kuanza maandamano kuanzia jumatatu ijayo.
Bodi ya wanaphamasia yalaumiwa kwa ongezeko la dawa ghushi
Bodi ya wanaphamasia nchini imelaumiwa kutokana na ongezeko la dawa ghushi na ghali mno zinazohatarisha maisha ya wagonjwa kando na kuathiri uchumi wa taifa.Waziri wa Afya Sicily Kariuki ameonya kwamba hawatosita kuwachukulia hatua wote walio na vibali vya kumiliki maduka ya kuuza dawa.
Mkutanao wa KNUT na TSC wagonga mwamba
Mkutano kati ya Chama cha waalimu nchini KNUT na mwajiri wao TSC uliokuwa ukiendelea mjini Naivasha umegonga mwamba. Hii ni kufuatia ripoti za tofauti kati ya pande hizo, baada ya waakilishi wa KNUT kuondoka kwenye ukumbi wa mazungumzo.
Kamati ya Bunge kuzuru vyoo vya wabunge
Kamati ya Mamlaka kuzuru vyoo vya wabunge wanawake kubaini ukweli
Imeadikwa na Beatrice Dama.