Story by Mwahoka Mtsumi –
Mama wa taifa Bi Margaret Kenyatta ameongoza halfa ya maadhimisho ya kimataifa ya kutokomeza fistula ya uzazi ambayo imesababisha changamoto nyingi kwa akina mama na wasichana katika bara la afrika.
Akizungumza wakati wa halfa hiyo ilioandaliwa katika majengo ya hospitali ya kitaifa Kenyatta jijini Nairobi, Bi Margaret ametoa wito wa juhudi endelevu za kutokomeza fistula ya uzazi.
Mama wa taifa amesema mwanamke yeyote anayesumbuliwa na maradhi hayo anapaswa kutibiwa mara moja ili kujenga afya yake na kuungana tena na jamii.
Kwa upande wake Katibu katika Wizara ya Afya nchini Dkt Susan Mochache, ameahidi kwamba serikali itahakikisha inawekeza mikakati muafaka ya kumaliza kabisa fistula ya uzazi nchini kabla ya mwaka wa 2030.