Mama wa aliyekuwa mwimbaji wa injili nchini Nigeria Osinachi Nwachukwu, Caroline Madu, ndiye shahidi mkuu katika kesi ya Nwachukwu, mume wa marehemu binti yake.
Mama huyo ameielezea mahakama maisha aliyoyapitia binti yake wakati wa uhai wake na ndani ya ndoa na Peter Nwachukwu kabla hajafa.
Mume wa marehemu Osinachi ‘alimnyanyasa binti yake na kusababisha kifo chake’, Caroline Madu aliiambia Mahakama Kuu ya Abuja siku ya Jumatatu.
Kifo cha Osinachi Nwachukwu kilichotokea Aprili 2022, kilizua ghadhabu kote nchini Nigeria na Afrika kwa jumla baada ya familia yake kudai kuwa alikabiliwa na ukatili wa majumbani kupitia mikono ya mume wake Peter Nwachukwu ambaye sasa anakabiliwa na mashtaka 23 kuhusiana na mauaji ya bila kukusudia yaliyosababisha kifo cha mwimbaji huyo kama ikiwemo;
- Madai ya kwamba Peter alimfukuza Osinachi kwa nguvu kutoka kwa nyumba yake ya ndoa na kitendo hicho ni kinyume cha Sheria ya Unyanyasaji dhidi ya Watu, Sheria ya VAP (Marufuku), ya 2015.
- Na kumsukuma huko kwa nguvu mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka kwenye gari linalotembea.
- Anashtakiwa kwa kufanya mauaji bila kukusudia chini ya kifungu cha 104 na 379 cha Sheria ya Utawala wa Haki ya Jinai, 2015. Makosa hayo ni kinyume na kifungu cha 221 cha Kanuni ya Adhabu na adhabu yake ni kifo.
- Mshtakiwa alimnyima Osinachi uhuru wake wa binafsi huku akimzuia kutembea na kumfungia nyumbani. Sheria, 2015.
- Mshitakiwa amemnyima Osinachi kupata pesa zake ili aende hospitali na kuzitumia katika mahitaji ya nyumbani huku akimlazimisha kuomba na kukopa. Mume wa Osinachi alimtenga kwa nguvu na na familia yake kwa kumzuia mama yake na ndugu zake kutembelea nyumbani kwao. Nwachukwu anadaiwa kumpiga mwimbaji huyo na kurekodi sauti ya kulia.
Madam Madu aliangua kilio wakati akisimulia jinsi “Peter alivyoenda nyumbani kwake akijificha kama mwinjilisti”.
Ni “kumuiba na kumuua binti yangu” anaiambia mahakama.
Madam Madu anasema tangu alipoolewa kwa miaka 14,alirudi nyumbani pale akiwa mgonjwa tu.
Aidha, Mama huyo pia alitoa ushahidi mbele ya mahakama akisema Peter hakumruhusu kumtembelea binti yake kwa sababu anamwita mchawi.
Pia hakumruhusu mwimbaji marehemu Osinachi kuhusiana na ndugu yake yeyote, anadai.
Mama huyo alisema kwamba ugonjwa pekee ambao binti yake alikuwa nao ulikuwa ni vidonda vya tumbo.
Mama huyo ameongeza kwa kusema yeye alienda sokoni kununua bidhaa na kumpa mdogo wake Osinachi kwenda kumpadada yake baada ya kumwambia kuwa alikuwa na njaa.
Akiwa nyumbani, mume wa Osinachi alianza kumnyanyasa mvulana huyo, anaiambia mahakama.
Dada wa Osinachi pia atatoa ushahidi mbele ya mahakama Jumatatu ya Juni 20, 2022.
Alielezea korti kwamba Peter alimchukulia Osinachi kama mnyama na kumpiga.
Baada ya kuhojiwa, wakili wa utetezi, aliiomba mahakama kuahirisha kesi.
Hata hivyo, polisi wa Nigeria walimkamata Nwachukwu na bado yuko kizuizini kabla hata ya kufunguliwa mashtaka.