Msanii wa mziki wa kisasa wa kimijikenda Nzingo Kalama maarufu kama Mama Burudisho ameaga dunia.
Kulingana na msanii wa mziki wa Bango, Stella Mbeyu, ambaye Mama Burudisho ni mamake mdogo ni kwamba marehemu alifariki tarehe 26 Disemba 2018 akipokea matibabu katika hospitali kuu ya kaunti ya Kilifi.
Marehemu atazikwa tarehe 12 Januari 2019, nyumbani kwao Gandini, Chonyi.
Mama Burudisho alivuma kwa vibao kama vile Becha, Mwafrika, na kibao Ndarya na munyu pkwanza.
Taarifa na Dominick Mwambui.