Familia moja katika mtaa wa Kwa Karanja mjini Kwale imepigwa na butwaa baada ya kupata kipande cha nyama kilicho na maandishi ya Quran.
Kulingana na mama wa familia hiyo amabye hakutaka kutambulika ni kuwa alipata kipande hicho pale alipokuwa ana andaa chakula cha jioni.
“Nyama zilikuwa kwenye sufuria nilipokiona kipande hicho kilichokuwa na maandishi ya Quran. Mumewangu na watoto walindelea na mlo baada ya kuupika lakini nilishindwa kula,” amesema Mama huyo.
Ameongezea uwa kipande hicho cha wanyama amekiweka kwa siku tatu nab ado hakijaanza kuoza wala kuonyesha dalili ya kuharibika.