Story by Ali Chete –
Mali ya thamani isiyojulikana imeteketea moto baada ya nyumba ya vyumba 11 kushika moto katika kijiji cha Mbuyuni eneo la Chaani kaunti ya Mombasa.
Akithibitisha kutokea kwa mkasa huo, Chifu wa eneo la Chaani Ben Mutunga Valasa amesema juhudi za wazima moto kuukabili moto huo ziligonga mwamba kutokana na ukosefu wa barabara ambayo imezibwa na vibanda vya wafanyibiashara.
Valasa hata hivyo ameitaka serikali ya kaunti ya Mombasa kuzifanyia ukaguzi barabara zote eneo hilo.
Kwa upande wake Hillary Utsimi ambaye ni muathiriwa wa mkasa huo amesema huenda chanzo cha moto huo ni hitilafu za nguvu za umeme.