Taarifa na Mercy Tumaini.
Mombasa, Kenya, Juni 26 – Mali ya thamani isiojulikana imeangamia baada ya bweni moja la shule ya upili ya wavulana ya St Georges eneo la Kaloleni kaunti ya Kilifi kuchomeka.
Akithibithisha kisa hicho mkurugenzi wa elimu eneo la Kaloleni Khalif Hirey amesema kuwa wanafunzi walikuwa madarasani wakati wa mkasa huo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Mwamuye Bashir Omar amewataka wazazi waliona wanafunzi katika shule hio kutokua na hofu akisema wanafunzi wote wako salama.
Hata hivyo afisa mkuu wa polisi eneo la Kaloleni Kennedy Osando amesema uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha moto huo.