Taarifa na Mwanaamina Faki
Mali ya thamani isiojulikana imeteketea moto katika eneo la Diani kule Ukunda kaunti ya Kwale.
Hamisi Mwero mkaazi wa eneo hilo, amesema hakuna kilichoweza kuokolea wakati wa mkasa huo wa moto licha ya juhuzi zao za kujaribu kuuzima moto huo ambao umetekeleza nyumba nzima.
Mwero amesema japo chanzo cha moto huo hakijabainika lakini polisi tayari wamefika kwenye eneo la mkasa kuanzisha uchunguzi.
Magari ya wazima moto kutoka kaunti ya Kwale yaliwasili kwenye eneo la mkasa huo kusaidia kuuzima moto huo licha ya kufika kuchelewa.