Story by Gabriel Mwaganjoni –
Mali ya thamani ya maelefu ya pesa imeteketea usiku wa Jumamosi baada ya soko la Marikiti katika kaunti ya Mombasa kuchomeka.
Japo chanzo cha moto huo hakijabainika wazi, wazima moto kutoka kaunti ya Mombasa walifika sokoni humo na kupambana na moto kwa ushirikiano na wakaazi wa kaunti hiyo wakati tayari mali nyingi ilikuwa imeharibiwa.
Viongozi mbalimbali kutoka kaunti ya Mombasa wakiongozwa na Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharrif Nassir ametaka uchunguzi wa haraka kuanzishwa ili kubaini chanzo cha moto huo ambao umesababisha hasara kubwa wa wafanyibiashara wa soko hilo.
Tukio hilo limejiri ndani ya juma moja baada ya soko kuu la Kongowea katika kaunti hiyo kuchomeka na mali ya maelfu ya pesa kuharibiwa.