Story by Gabriel Mwaganjoni –
Wafanyabiashara katika soko kuu la Kongowea kaunti ya Mombasa wanaendelea kuhesabu hasara baada ya mali yao kuteketea moto usiku wa Jumanne.
Mmoja wa wafanyabiashara hao Rose Okwaro amesema wameathirika pakubwa kufuatia mkasa huo na hadi sasa hawana cha kutegemea.
Kwa upande wake, Rose Ntamre amesema huenda kuna mvutano sokoni humo kwani ni mara ya pili kwa soko hilo kuteketea ndani ya kipindi cha miaka miwili huku moto huo ukianzia eneo la kuuza nguo kuu kuu maarufu mitumba.
Baadhi ya Wafanyabiashara hao akiwemo Patricia na Caroline Awuor, wameomba msaada ili wazifufue upya biashara zao baada ya kuteketea moto.
Moto huo mkubwa uliteketeza eneo la kuuzia mitumba hali iliyopelekea mali ya thamani ya mamilioni ya pesa kuteketea na kuwasababishia wafanyabiashara hao hasara kubwa, japo hadi sasa kini cha moto huo kingali kitendawili.