Story by Gabriel Mwaganjoni
Mali ya thamani ya maelfu ya pesa imeteketea baada ya moto kuteketeza jumba la kibiashara katika mzunguko wa barabara ya Fontanella katikati kwa mji wa Mombasa.
Moto huo umetajwa kuchangiwa na hitilafu za nyaya za kusambaza umeme katika jumba hilo la ghorofa tatu na lililo na vyumba vingine vya chini ya ardhi.
Maduka yaliyoripitiwa kuteketea katika jumba hilo ni pamoja na lile la kampuni ya mawasiliano nchini Safaricom, taasisi ya kifedha, kituo cha kuadilisha sarafu za kigeni, maduka ya vifaa vya eletroniki, miongoni mwa maduka mengine.
Imewachukua wazima moto kutoka serikali ya kaunti ya Mombasa masaa mengi kuukabili moto huo, shughuli iliyokabiliwa na vikwazo vingi hasa ikizingatiwa kwamba moto huo umeanza sehemu ya chini ya ardhi ya jengo hilo kabla ya kupanda juu ya ghorofa hizo.
Hata hivyo, moto huo umethibitiwa baadaye na wamiliki wa maduka kuamrishwa kusalia nje ya jumba hilo kadri juhudi za kukagua usalama wa jumba hilo zilipokuwa zikiendelezwa na watalaam wa mikasa ya moto.