Picha kwa hisani –
Gavana wa kaunti ya Makueni Profesa Kivutha Kibwana na mwenzake wa kaunti ya Machakos Dkt Alfred Mutua wamebadilisha msimamo wao na kuanza kuunga mkono mchakato wa BBI.
Akihutubia wanahabari gavana wa Makueni Kivutha Kibwa amesema wamegundua BBI ina manufaa kwa wakenya na iwapo itaungwa mkono maendeleo yatafanikishwa hadi mashinani.
Kibwana amesema ana imani kwamba wajumbe katika bunge la kaunti ya Makuani wataupitisha mswada wa BBI kwani wamekuwa mashinani kuwahamisisha wananchi kuhusu umuhimu wa BBI.
Kwa upande wake Gavana wa Machakos, Dkt Afred Mutua amesema ana matumaini makubwa kuwa mswada huo utapitishwa katika mabunge yote ya kaunti humu nchini akisema kaunti ya Machakos imeridhishwa na yaliomo ndani ya ripoti BBI.